Meneja wa wasanii wa Tip Top na Diamond, Babu Tale amezungumza kuhusu ‘bifu’ linaloendela kati yake na msanii Baghdad, ambalo limepelekea kwa sasa kutolewa kwenye group la Whatsapp la wasanii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Babu Tale alisema: Sitaki kumpa promo hiyo, akitaka promo aje nimpe promo sio hiyo.
Pia Tale amekiri kutolewa kwenye group hilo, na kusema kuwa kabla yeye hajatolewa alishawatoa wasanii wote anaowasimamia na kisha yeye akatolewa.
“Mimi nimewatoa watu wangu, wasanii wangu wote ambao nawasimamia mimi halafu baadaye wasanii ndio wakanitoa”, alisema.
0 comments:
Post a Comment