Kwa hili analolifanya Ronaldo ni kweli anakaribia kuondoka Madrid?



Kwenye mchezo wa soka kwa sasa ukiulizwa utaje wachezaji bora, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi lazima utawataja kwenye list yako.



Vyombo vingi vya habari duniani vimeripoti kuwa mwishoni mwa msimu, timu ya Real Madrid itawauza baadhi ya nyota wake waliosajiliwa kwa kiasi kikubwa na kulipwa mishahara mikubwa. Kati ya wachezaji ambao wanasemekana ni pamoja na Ronaldo, Toni Kroos, Isco na James Rodriguez.

Ronaldo ameiweka sokoni nyumba yake anayoishi yenye vyumba saba kwa thamani ya paundi milioni 4.9, lakini pia inasemekana Ronaldo ameiweka sokoni na nyumba ya mama yake ambayo ina thamani ya paundi milioni 2.5.

‘Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja’, tusubiri tuone kwani hata mwaka 2009 taarifa za kuhama kutoka Manchester United kwenda Madrid zilikuwa kama masihara wakati mwenyewe alikuwa Marekani kwenye mapumziko yake ya msimu mpya.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment