Chege asema madai ya kuwa Madj wa bongo hawapigi ngoma za nyumbani sio ya kweli




Msanii wa Kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema kuwa madai ya kuwa Madj wa bongo hawapigi ngoma za wasanii wa nyumbani sio ya kweli.


Akizungumza katika kipindi cha Mkasi TV cha East Africa Television hivi karibuni, Chege amesema Madj wa bongo wanapiga sana nyimbo za wasanii wao wa ndani.

“Hapa sio kweli, hamna Dj huyo, sio kweli wanapiga ngoma zote lakini wanapiga ngoma nyingi za nje kuliko wao wanavyopiga za kwetu na sio kwamba hawapigi za kwetu. Madj wetu wanapiga sana kazi zetu tusiwalaumu, mimi naenda Club na ngoma nazisikia,” alisema Chege baada ya kuulizwa kwanini Madjs wa bongo wanapiga ngoma nyingi za nje kuliko za ndani.

Pia muimbaji huyo anayefanya vizuri na video yake ya wimbo Sweety Sweety, alisema kama ni kufungiwa ngoma za nje zisichezwe hapa nchini basi zifungiwe za wasanii wa Marekani na sio za wasanii wa Afrika.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment