Mwana FA amesema imefika wakati muziki wa Nigeria unaabudiwa hapa Tanzania lakini yeye anaamini nyimbo zao ni takataka.
Akiongea jana kwenye kipindi Ladha 3600 cha EFM, FA alisema ndiyo maana wasanii wengi wanaposema wanataka kufanya collabo ya kimataifa, humaanisha ‘collabo ya Kinaijeria.’
“Tumefika mahali huu muziki unaabudiwa, wa Kinaijeria wakati kiukweli ni shit music,” alisema FA.
Aliongeza kuwa ndiyo maana yeye hana mpango wa kufanya collabo yoyote na msanii wa nje kwa sasa, hasa kutoka nchini humo.
“Muziki ninaoufanya naufanya kwaajili ya watu wangu wa hapa, mimi nauza mashairi , lugha ninayoitumia na presentation ninayoifanya na jinsi ambavyo watu wanataka warelate na muziki wangu ni mazingira yanayonizunguka mimi moja kwa moja. Kwahiyo kama collaboration zitakuja zije, nikitaka kufanya na wasanii wa nje wala sio kitu kigumu kabisa lakini sio kitu ninachokifiria sana sababu sio direction ya muziki wangu ninaotaka kuipeleka,” aliongeza.
Credit bongo5
0 comments:
Post a Comment