Godzilla adai haitaji tena kolabo na msanii yeyote, ‘sitaki kuwa mtumwa’



Msanii Godzilla amesema kwa sasa hatofanya kolabo na msanii yeyote, kwani anahitaji kusimama mwenyewe kwenye kazi zake.



Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Godzila amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kwani hataki usumbufu na msanii yeyote.

“Zilla ana ndoto za kufanya kazi na zilla miaka yote hii, jambo la kwanza sitaki disapointment kwenye kazi yangu, muziki unahitaji uhuru, muziki unahitaji muda, unahitaji utulivu wa akili, nikifanya kazi na wewe kukutafuta nikuhitaji tena kwa namna moja au nyingine itanigharimu, I dont need people till I die, with anybody labda itokee tu, si matusi si dhambi, kila binadamu ana choice zake za life”, alisema Godzilla.

Pia Godzilla amesema kwa kufanya hivyo kutaweza kumsaidia kukaza zaidi kwenye game, na kuzidi kufanya vizuri kwa kazi zake mwenyewe bila kumtegemea mtu.

“Sanaa yangu nitakuwa nastrugle, naweza kuimba, naweza kurap, naweza kufree style, nimetengeneza hit song hadi za kuimba peke yangu, nahitaji kolabo ipi tena, nahitaji kolabo na mimi, sitaki kuwa mtumwa, yani ukiwa na sanaa nzuri hewani hutakiwi kuwa mtumwa, na hiyo inakuongezea utafutaji mara mbili, kwamba si nimefanya kazi hii sina kolabo sina nini, kwa hiyo muhimu hii kazi iende kwahiyo ukiwa studio hubweteki”, alisema Godzilla.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment