Mr Blue afunguka kuhusu Sugu kumuibia ngoma yake inayoitwa Freedom

post-feature-image


Sugu ameachilia video ya Freedom na audio yake ilitoka sikuchache zilizo pita. Kumbe ngoma hiyo ilikuwa ya Mr Blue. Kwenye ukurasa wake wa instagram Mr. Blue ameandika ujumbe huku akiomba mashabiki wake wamshauri nini afanye, kwani Mr. Sugu anamuheshimu kama kaka yake.


Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa "Freedom" tulifanya pale kwa Makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu, je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn...mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu....????”, aliandika Mr. Blue.

Wimbo huo wa 'Freedom' ambao tayari upo kwenye mitandao, umeonekana ukiandikwa ni Mr. Blue ft Sugu, huku mwengine ambao umeshafanyiwa video unaonekana ukiandikwa wa Sugu ft Lizzy.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment