Nimewekeza pesa nyingi sana kwenye muziki wangu – Vanessa Mdee


Msanii wa muziki wa kike anayefanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Niroge’, Vanessa Mdee, amesema uwekezaji aliyoufanya kwenye muziki wake ndio kitu kinachomweka vizuri.






Akizungumza na BBC Jumanne hii, Vanessa amewataka wasanii wenzake kuwekeza kwenye muziki wao kwa kuwa hiyo ni biashara kama biashara nyingine.

“Kitu ambacho niliongeza kwenye muziki wangu ambacho kiliweza kunipush zaidi ni kuwekeza kwenye muziki, nimewekeza pesa nyingi kwenye muziki, mimi nachukulia hii kama biashara nyingine,” alisema Vanessa.

“Nimewekeza pesa, akili, man power yaani nimeajiri Watanzania ili kuendeleza muziki wa Vanessa, sio kitu ambacho naweza kufanya mimi peke yangu, kuna team saa zote inafikiria nini tufanye ili tutengeneze pesa. Nawashauri wasanii wenzangu wawekeze kwenye muziki, matokeo watayaona muda mfupi tu,” aliongeza Vanessa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment