Mama mzazi wa msanii wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amewasili Jijini Dar es salaam Jumatatu hii kwa ajili ya mazishi ya mwanae aliyefariki dunia Jumamosi hii katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mama yake Ndanda Kosovo (katikati) akilia kwa uchungu
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii shemeji wa marehemu, Mama Fiji, akiwa Kinondoni Ananasif pahala ambapo taratibu za mazishi zinafanyika, amesema taratibu za mazishi zinaendelea vizuri baada ya kuwasili kwa mama mzazi wa Ndanda Kosovo.
“Tunashukuru Mungu mama amekuja jana usiku. Kwa hiyo taratibu ya mazishi zipo pale pale, sema leo jioni tutakaa tena na kupanga vitu vidogovidogo,” alisema Fiji.
Pia Fiji alisema Mama Ndanda Kosovo, amefurahishwa na upendo wa Watanzania jinsi ambavyo wanasupport taratibu mbalimbali za mazishi ya mwanae.
“Mama amefika salama ingawa ana uchovu wa safari pamoja na majonzi. Lakini anawashukuru sana Watanzania kwa upendo wao mpaka sasa.,” alisema Fiji.
Ndanda Kosovo atazikwa Jumatano hii katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Watoto wa Ndanda Kosovo wakicheza
Watoto wa Ndanda Kosovo wakiwa na bibi yake
Ndugu wa Ndanda Kosovo
Sehemu ambayo ataagwa Ndanda Kosovo
Credit Bongo5
Credit Bongo5
0 comments:
Post a Comment