Rammy Galis kuondoka leo kwenda Lagos kumalizia filamu mpya ‘Red Flag’



Muigizaji wa filamu nchini, Rammy Galis, anatarajia kuondoka Jumanne hii kwenda Lagos, nchini Nigeria kwaajili ya kumalizia filamu yake mpya, Red Flag.



Filamu hiyo ni ya Kiingereza kitupu.

“Leo usiku muigizaji nyota Rammy Galis atapanda ndege kuelekea Lagos kumalizia movie ijulikanayo kama Red Flag ambayo ni script ya Kiingereza mwanzo mwisho,” Dr Almas ambaye pia ameshiriki kwenye filamu hiyo ameiambia Bongo5.

“Mimi pia nimefanya yangu humo na usiku pia nitakuwepo airport kumsindikiza. Director wa movie hii anatoka Australia, na kama utakumbuka Rammy Gals atakuwa msanii wa pili baada ya Kanumba kufanya hivyo,” ameongeza.

Rammy Galis amejichukulia umaarufu kwa uwezo wake mkubwa katika uigizaji. Filamu alizoigiza ni pamoja na Chausiku, Snitch, Malaika, Fan’s Death na zingine.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment