Baada ya kufanya vizuri kwenye verse za nyimbo zake akiwa mwenyewe, rapper Chemical anakaribia kuachia wimbo aliomshirikisha Fid Q.
Mmoja wa viongozi wa menejimenti ya Kazi Kwanza amesema ‘Tutaanza kuachia video ya wimbo wa Chemical aliomshirikisha Fid Q mwishoni mwa mwezi huu wa tano.’
“Sasa hivi tutakuja na style nyingine ya kuachia wimbo wa Chemical. Tutaanza kuachia video kwanza na baadaye itafuata audio. Wimbo unaofuata ni ‘Hero’ amemshirikisha Fid Q, na director wa video ya wimbo huo atakuwa Msafiri wa Kwetu Studio,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment