Mama yake Tupac, Afeni Shakur Davis afariki dunia


Afeni Shakur Davis, mama yake na hayati Tupac Shakur amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 69.



Mama huyo alipata mshtuko wa moyo Jumanne kabla ya kupelekwa hospitali alikopoteza maisha kabla ya saa nne na nusu usiku.

Shakur, aliyezaliwa kwa jina la Alice Faye Williams, alibadilisha jina lake baada ya kuhamia New York City na kujiunga na vugu vugu la Black Panther.

Tupac aliwahi kumuimbia mama yake huyo kwenye wimbo ‘Dear Mama’ wa mwaka 1995 akielezea shida za utotoni na alivyomheshimu mama yake.

“There’s no way I can pay you back/But the plan is to show you that I understand/You are appreciated,” alirap Tupac.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment