Davido aingia studio na Tinashe na Rae Sremmurd


Tangu asaini record deal na Sony Music, staa wa Nigeria, Davido amekuwa akijichanganya na mastaa wanaohit Marekani.



Hivi karibuni alishare picha kwenye Instagram akiwa na muimbaji mrembo, Tinashe, kitu kinachoonesha wazi kuwa wanatengeneza ngoma ya pamoja.



“How long will you wait … @tinashenow,” aliandika Davido kwenye picha moja akiwa na muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Tinashe Jorgenson Kachingwe na mwenye asili ya Zimbabwe.
“Can u make me feel like number 1 ??? @tinashenow,” aliandika kwenye picha nyingine.

Tinashe amehit sana Marekani na nyimbo zake kama 2 On, All Hands on Deck na Player aliyomshirikisha Chris Brown.



Pia Davido alishare picha akiwa na rappers ndugu, Khalif “Swae Lee” Brown na Aaquil “Slim Jimmi” Brown wanaounda kundi la Rae Sremmurd.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment