Kuna watu walinibania kufanya kazi na Koffi Olomide – AT



Muimbaji wa Mduara kutoka visiwani Zanzibar, AT anaamini ili muziki wa Tanzania ukue lazima kuwe na umoja na unafiki uishe.



AT amesema watu wenye roho mbaya wamejaa kwenye muziki wa Tanzania. Akiongea na Bongo5 AT amesema kuna mchongo aliowahi kuupata wa kufanya kazi na msanii wa DRC, Koffie Olomide lakini kuna watu walimbania ikashindikana.

“Nilikuwa na mchongo wa kufanya kazi na Koffi Olomide watu niliyowafuata wakanitosa kwa kuhofia wasanii wao watashuka. Wapo wenyewe wanajijua kabisa niliwafuata na wakaniyeyusha na mimi nawajua ni kitu ambacho huwa kinaniuma sana. Ndio maana leo nimeamua kusema ila wajue tu kuwa shetani huwa hafungwi jela,” amesema AT.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment