Mahakama ya kutatua mizozo ya kimichezo imempunguzia adhabu rais wa shirikisho la soka Ulaya, Michel Platini.
Awali Platini na Sepp Blatter walipewa adhabu ya kutojihusisha na michezo kwa kipindi cha miaka sita kutokana na kosa la ukiukwaji wa maadili ya sheria za FIFA. Baada ya kamati ya mahakama hiyo kukaa imefikia maamuzi ya kumpunguzia adhabu Platini kutoka miaka sita hadi kufikia miaka minne kutojihusisha na michezo.
Japo mara kadhaa wawili hao walikataa tuhuma hizo zinazowakabili, lakini pia Platini anajiandaa kustaafu wadhifa wake kama rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa).
0 comments:
Post a Comment