Lemonade ya Beyonce yakamata namba moja kwenye Billboard 200



Album ya sita ya Beyonce, Lemonade, imekamata nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200.



Album hiyo imeuza nakala za usawa wa 653,000 katika wiki iliyoishia April 28, kwa mujibu wa Nielsen Music.

Chati za Billboard 200 hutumia njia mbalimbali zikiwemo uuzaji wa kawaida wa album wa kawaida, track equivalent albums (TEA) na streaming equivalent albums (SEA).

Lemonade iliingia sokoni April 23 ikiwa na nyimbo 12 na zote zikiwa na video.

Album zote sita za Beyonce zimewahi kukamata namba moja kwenye Billboard 200. Zingine ni Beyonce (2013), 4 (2011), I Am… Sasha Fierce (2008), B’Day (2006) na Dangerously In Love (2003).




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment