Rais Magufuli aziagiza wizara kupunguza ajira kwa raia wa kigeni



Ni mara ngapi umeenda kwenye ofisi fulani hapa nchini na ukakuta asilimia 50 ya wafanyakazi ni raia wa kigeni?



Na kinachosikitisha zaidi ni kuwa mara nyingi wageni ndiyo wenye vyeo vya juu na hulipwa mishahara mikubwa. Hilo linaelekea kufikia mwisho kwasababu, Rais Dkt John Pombe Magufuli ameziagiza wizara zote kuhakikisha kuwa zinapunguza ajira kwa raia wa kigeni na kuwapa nafasi zaidi wazawa.

Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, May Mosi, Magufuli alidai kuwa kuna maeneo mengi ambayo yameajiri raia wa kigeni wakati ni kazi zinazoweza kufanywa na wazawa.

Alidai kuwa kama tatizo ni lugha iweje wachina wanafanya kazi nchini bila kujua lugha nyingine zaidi ya kwao na kwamba hata watanzania wasiojua Kiingereza wana haki ya kupewa ajira na wakawasiliana kwa lugha yao.

Katika hatua nyingine Magufuli aliagiza kupunguzwa kwa kodi ya mshahara (PAYE) kutoka asilimia 11 hadi 9 kuanzia kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017.

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yalifanyika kitaifa Dodoma.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment