Winga wa klabu ya Man United ya Uingereza Memphis Depay huenda ni kweli anaweza kuondoka katika klabu hiyo kuna tetesi kuwa kwa sasa anakosa furaha ndani ya Man United.

Memphis amewaduwaza mashabiki wake wengi hasa wa Man United wanaomfollow katika account yake ya Instagram, baada ya kuona winga huyo kaamua kufuta picha zote katika Instagram yake zinazohusu Man United ambazo aliwahi kupost na kubakisha moja akiwa na mpenzi wake pekee saivi Depay ndo mchezaji ambaye anaongoza kwa mauzo ya jezi yake namba 7 katika klabu yake na pamoja na ligi ya EPL kufanya ivyo kunaashilia kuwa huu huwenda ukawa msimu wake wa mwisho Man?.

Katika account yake ya Instagram ya Memphis amefollow watu 11 pamoja na account ya Man United pekee, hakuna mchezaji mwenzake wa Man United aliyemfollow, kitu ambacho kimeandikwa na mitandao mingi ya Ulaya kuwa huenda winga huyo anataka kuondoka Man United
0 comments:
Post a Comment