Klabu ya Leicester City hadi sasa wamebakiwa na point mbili tu pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge.

Leicester walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla ya kusawazisha kupitia kepten wao Wes Morgan dakika ya 17.
kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na alama 77. Claudio Ranieri huyo akisisitiza kuwa hawakufuata kikombe OT bali kucheza mchezo safi lakini Man U walikua wazuri zaidi yao.

Matokeo mengine Liverpool walichapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton.

0 comments:
Post a Comment