Baada ya Swizz Beatz Wizkid aingia studio na French Montana


Wakati ambapo wasanii kibao wa Afrika wanatoa jasho kutafuta collabo na wasanii wakubwa wa Marekani, kwa Wizkid mambo ni tofauti na rahisi kabisa.


Milango inazidi kufunguka kwa mkali huyo huku collabo zikimfuata kila kukicha.

Hivi karibuni alishare picha akiwa na producer mahiri wa Marekani, Swizz Beatz kuashiria kuwa wamekutana kufanya kazi ya pamoja. Beatz pia alipost picha hiyo Instagram akiwa na mkali huyo.

Lakini sasa imebainika kuwa staa huyo ameingia tena studio kufanya ngoma na rapper French Montana. Muongozaji wa video wa label ya MMG, Spliff ameweka video Instagram akiwa studio na Wiz na kuandika kuwa ni ngoma aliyofanya na Montana.

Wakati collabo hizo zikiwa jikoni, wimbo wa Drake, One Dance alioshirikishwa, bado umekamata namba moja kwenye chat za Billboard Hot 100.

Mwaka huu staa huyo anachuana na mastaa wengine akiwemo Diamond, AKA, Cassper Nyovest na Yemi Alade kwenye tuzo za BET zinazotolewa wikiendi hii.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment