Dayna Nyange: ‘Angejua’ imevunja rekodi ya ‘Nivute Kwako’



Dayna Nyange amesema kuwa tangu alipoachia wimbo wa ‘Nivute Kwako’ hakuwahi kuachia wimbo uliokuwa juu zaidi ya wimbo huo lakini wimbo wa’Angejua’umevunja rekodi hiyo.


Akiongea na Bongo5, Dayna amesema kuwa wimbo wa ‘Angejua’ umemsaidia zaidi ya nyimbo alizowahi kuzitoa hapo nyuma.

“Angejua ni wimbo ambao kiukweli umefanya vizuri na umenisaidia sana. Nilikuwa nikiachia nyimbo na kupata show lakini zilikuwa hazijafanikiwa kufika kwenye peak nzuri. Kwa sababu tangu nimeachia wimbo wa ‘Nivute Kwako’ sikuwahi kuachia wimbo ulioweza kuupiku lakini ‘Angejua’ ni wimbo ambao umefanikiwa kufanya vizuri zaidi ya ‘Nivute Kwako’,” amesema Dayna.

“Hiyo inatokea kwa kila msanii sio kwa Dayna pekee. Kuna wakati unaweza ukatoa wimbo ukawa mkubwa zaidi ukashindwa kutoa wimbo mwingine wa kuuzidi wa mwanzo,” aliongeza.

Credit Bongo 5


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment