Huenda Pacquiao akarejea tena ulingoni October


Manny Pacquiao alitangaza kustaafu masumbwi, lakini promota wake tayari ameshaweka mpango wa bondia huyo kuingia ulingoni tena.



Promota, Bob Arum ameripotiwa akisema kuwa tayari Oct. 15 imewekwa kama siku ambayo Pacquiao atarajea ulingoni na tayari wapinzani wake wamejulikana.

Arum amewataja mabondia hao kuwa ni Terence Crawford, bingwa wa mkanda wa WBC uzito wa welterweight, Danny Garcia na Adrien Broner.

Pacquiao, ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa seneta nchini Ufilipino, anatarajia kukutana na Arum wiki zijazo kuzungumzia mustakabali wake ulingoni.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment