Msanii wa muziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanzisha label yake mpya ‘Shilole Entertainment’ ambapo pia amemsaini msanii chipukizi aitwae ‘Amaselly’.
Shilole na msanii wake mpya aitwae Amaselly
“Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema Shilole.
Shilole na Amaselly
Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo mazuri.
Hii hapa chini ni moja kati ya kazi za msanii huyo ambayo aliifanya kipindi cha nyuma
0 comments:
Post a Comment