Mr Nice aachia albamu mpya ‘Kioo’, auza nakala 5000 nchini Kenya pekee



Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice Jumatano hii aliachia albamu yake mpya ‘Kioo’ ambapo mpaka sasa tayari ameshauza nakala 5000.




Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii akiwa nchini Kenya, Mr Nice amesema albamu hiyo kwa sasa inapatikana nchini Kenya pekee.

“Kama nilivyohaidi kuwa sitembei na single kama wasanii wengine, natembea kiutuuzima zaidi kwa kutoa albumu,” alisema Mr Nice. “ahadi nimetimiza na mzigo umeingia sokoni rasmi na tayari nakala 5000 zimenunuliwa fasta ndani ya Kenya pekee,”

Aliongeza, “Nipo Kenya sasa katika tour kubwa kabisa ya kuitangaza albumu hii mpya na nina zaidi ya mwezi na nusu sasa ni show kwa kwenda mbele, after Kenya then ni Uganda halafu Rwanda na kwingineko kama ilivyo kawaida yangu, makoloni yangu yalipo napajua mimi mwenyewe. Nawashukuru sana mashabiki wa huko nyumbani Tanzania kwa kunisapoti na kuweza kunitia nguvu na hamasa kwa kipindi chote nilichokuwa nimetulia nikiandaa mambo na hatimae wakati umewadia na ahadi nimeitimiza sasa,”

Source Bongo 5


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment