Professor Jay kuvunja ukimya, apanga kuipeleka brand ya Professor Jay kimataifa



Mbunge wa Mikumi na msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amesema tayari ameshafanya alichoagizwa na wapiga kura wake wa jimbo lake la Mikumi, na kwa sasa alichobakiza ni kukata kiu ya mashabiki wa muziki wake.



Akiongea na Bongo5 wiki hii, Professor Jay amesema kwa sasa hivi anajipanga kuupeleka muziki wake kimataifa zaidi.

“Kuhusu mashabiki wangu nimaambie tu kile kilio chao cha muda mrefu cha kunimis na mimi nimewamis, ni hivyo tu nilibanwa na majukumu ya kuwatumikia wananchi wa Mikumi, lakini naweza kusema nimewahudumia vya kutosha na wamenielewa na wameona dhamira yangu ya dhati ya kuwatumikia. Kwa hiyo nitaiba muda niweze kuendelea na muziki, kwa sababu hata wananchi wa Mikumi niliwaambia, nitaendelea kufanya muziki kwa sababu hichi ni kipaji nilichopewa na Mungu,” alisema Professor Jay.

Aliongeza, “Kwa hiyo mashabiki wangu waelewe napata muda sasa, japo bado bungeni kuwa na mambo mengi, lakini napata muda na muda sio mrefu nitazungumza nao kwa kuachia track ambazo watazielewa kwa sababu nataka kufanya muziki wa kwenye level nyingine, yaani wa hali ya juu zaidi nataka nifanye brand ya Professor Jay iende kimataifa zaidi kwa kufanya muziki wa kiwango cha juu zaidi,

Source Bongo5
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment