Malaika amesema mashabiki wake watarajie mabadiliko makubwa kwenye muziki wake mpya. Hivi karibuni muimbaji huyo alidai kupata uongozi mpya wa kusimamia kazi zake wenye makazi yake Norway.
“Ni kweli kuna watu kutoka Norway wapo tayari kufanya kazi na mimi kwahiyo kuna project zingine mpya zinakuja mashabiki wangu wataona tu mabadiliko katika kazi zangu. Sasa hivi wakae tayari kwa video yangu mpya ya wimbo Nawararuararua inatoka muda wowote.”
0 comments:
Post a Comment