Barcelona yaingiza faida ya Euro milioni 29 kwenye msimu wa 2015/16
Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania imetangaza kukusanya kiasi cha Euro milioni 679 kwenye msimu wa mwaka 2015/2016 wa ligi ya La Liga ya nchini humo.
Makusanyo hayo yaliyofanywa na timu hiyo yamevunja rekodi baada ya kupata faida ya kiasi cha Euro milioni 29 ikiwa tayari imeshakatwa makato yote.
Hivi karibuni jarida maarufu duniani la Forbes liliitangaza klabu hiyo kuwa ni klabu ya michezo ya tatu duniani kwa kuwa na utajiri wa kiasi cha dola bilioni 3.55 huku namba moja ikishikiliwa na klabu ya Klabu ya NFL, Dallas Cowboys yenye utajiri wa dola bilioni 4 na namba mbili ikichukuliwa na mahasimu wao Real Madrid yenye utajiri wa dola bilioni 3.65.
Katika hatua nyingine klabu hiyo ya Barcelona inayomiliki uwanja wa Camp Nou imepanga kuufanyia upanuzi uwanja wake huo ili uweze kuingiza watu wengi zaidi tofauti na ilivyokuwa sasa unaingiza mashabiki 99,354.
0 comments:
Post a Comment