Nikki wa Pili ataka elimu ya sanaa ifundishwe mashuleni


Msanii wa Kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameitaka serikali kuangalia suala la kutoa elimu ya sanaa katika shule za ngazi za chini na sio kwenye elimu ya juu pekee kama ilivyosasa.



Rapper huyo amesema kuwa elimu ya sanaa inapaswa ifundishwe darasani kuanzia chekechea mpaka form six.

“Nakumbuka zile takwimu za BASATA zinazo sema Tanzania inakadiriwa kuwa na wasanii milioni 10. Lakini mbona sanaa siioni katika mitaala ya elimu ya umma kuanzia chekechea mpaka form 6. Lakini kuna chuo cha Bagamoyo na Mlimani kuna kitivo cha sanaa sasa hii si ajabu unaanzaje kujifunzia sanaa chuo jamani?,” alihoji Nikki wa Pili kupitia instagram.

Aliongeza, “”Waeshimiwa wote mliopigiwa kampeni na wasanii, hebu jiulizeni hivi hasa wasanii katika mfumo wenu wa elimu, wao wako wapi. siyo tu kusema wasanii wanatutangaza kimataifa, wakati mfumo wenyewe wa elimu wa kitaifa hauitambui sanaa. Ama kusema wasanii hawana maadili, sanaa tunajifunzia magetoni, mitaani, youtube huko kote hamna maadili. Tungejifunzia darasani huenda kungekuwa na somo la sanaa na maadili. kama tu unavyo jifunza Procurement Ethics…..au maadili ya udaktari,”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment