Ukaguzi wa pili wabaini watumishi hewa 315 Morogoro.






Idadi ya watumishi hewa katika mkoa wa Morogoro imefikia 315 ikilinganishwa na 122 waliokuwa wamegundulika awali,baada ya kufanyika kwa uhakiki wa kina wa awamu nyingine katika wilaya zote saba zilizopo mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe amesema awali walipokea ripoti ya ukaguzi ambayo hawakuridhishwa nayo hivyo kuamua kufanya ukaguzi kwa mara ya pili na kugundua mkoa una watumishi hewa 315 huku wilaya ya Kilosa ikiongoza kuwa na idadi kubwa ya watumishi hewa 98,Kilombero 48, Morogoro vijijini 38,Mvomero 20,Gairo 13 na Malinyi saba,huku Ofisi ya mkuu wa mkoa na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kukiwa na watumishi hewa watano.

Kuhusu madawati,mkoa wa Morogoro umefanikiwa kuondoa tatizo la uhaba wa madawati kwa shule za sekondari kwa kufikia zaidi ya asilimia 100, wakati kwa shule za msingi ikifikia asilimia 95,hivyo Dk Kebwe kutumia fursa hiyo kuwaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha hadi kufikia Julai 15 wawe wamemaliza tatizo hilo.

Katika uhakiki huo,imebainika shilingi bilioni 2.2 zimelipwa kwa watumishi hao hewa huku milioni 42.8 zikiwa tayari zimerejeshwa.

Credit ITV
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment