Usajili wa Pogba kwenda Manchester United kukamilika ndani ya masaa 48 yajayo


Klabu ya Manchester United inatarajiwa kumsaini kiungo wa Juventus Paul Pogba ndani ya masaa 48 yajayo baada ya kukubali kulipa ada ya wakala wake.




Taarifa za ndani ya klabu hiyo zimedai kuwa tayari zimeshakubaliana na Juventus kwa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambaye anatarajiwa kufanya vipimo vya afya yake muda wowote huko nchini Marekani alipokuwa kwa kwenye mapumziko yake ya kujiandaa na msimu mpya.

Pogba anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa ndiye mchezaji ghali zaidi kuuzwa kweye tasnia ya soka huku ikikadiriwa kuwa United wamekubali kulipa kiasi cha zaidi ya paundi milioni 100 ili kuipata saini ya mchezaji huo mwenye miaka 23 anayewaniwa na timu nyingine ya Madrid.

Aidha imedaiwa kuwa wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola anadaiwa ndiye chanzo cha kuchelewesha dili la usajili wa mchezaji huyo kwa kutaka kulipwa kitita cha paundi milioni 25 nje ya pesa za usajili wa mchezaji huyo.

Pogba anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu hiyo na kupokea mshahara wa paundi 290,000 kwa wiki na atakuwa ni mchezaji wa nne kusajiliwa chini ya kocha mpya, Jose Mourinho akiwa mpaka sasa kasha msajili Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment