‘Views’ ya Drake yashika namba 1 kwenye Billboard Top 200 kwa wiki 9 mfululizo
Albamu mpya ya Drake ‘Views’ imeendelea kushika namba moja kwenye chati za Billboard Top 200 kwa wiki ya tisa mfululizo.
‘Views’ iliishusha kwenye chati hizo albamu ya Eminem ‘The Marshall Mathers LP’ iliyotoka mwezi Mei, 2000 na kushika namba moja kwenye chati hizo kwa wiki sita mfululizo. Lakini albamu ya MC Hammer ya mwaka 1990 ‘Hammer Don’t Hurt Em’ ndiyo inayoongoza kwa kuweka rekodi ya kushika namba moja kwenye chati hizo kwa wiki 21 mfululizo.
Kupitia kwenye akaunti ya Twitter, Billboard wamempongeza Drake kwa kuandika: “Congrats [email protected], whose ‘Views’ album taken the No. 1 spot for the ninthweek on the Billboard 200 chart.”
Drake alifanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni 1.04 ndani ya wiki mbili tangu alipoiachia albamu hiyo mwishoni mwa mwezi Aprili.
Hii ni top 10 ya albamu zinazoongoza kwenye chati ya Billboard Top 200 wiki hii:
1. Drake – Views – 111,000
2. Beyoncé – LEMONADE – 48,000
3. The Avett Brothers – True Sadness – 46,000
4. Twenty One Pilots – Blurryface – 38,000
5. Rihanna – ANTI – 37,000
6. Hamilton – 36,000
7. Adele – 25 – 33,000
8. Epic AF – 28,000
9. Red Hot Chili Peppers – The Getaway – 28,000
10. Meghan Trainor – Thank You – 27,000
0 comments:
Post a Comment