Baada ya kumkosa Jamie Vardy, Arsenal yapata pigo jingine kwa Riyad Mahrez
Klabu ya ligi kuu ya Uingereza, Leicester City, imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka minne mchezaji wao Riyad Mahrez aliyekuwa anawaniwa kwa karibu na timu ya Arsenal.
Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Algeria, amesaini mkataba huo ambao utamfanya kuichezea timu hiyo mpaka mwaka 2020 na amekuwa mchezaji wa pili wa timu hiyo kuongeza mkataba mpya huku akiiacha Arsenal njia panda kama alivyofanya Jamie Vardy mwezi uliopita.
Kupitia mtandao wa Twitter, Leicester City wameandika, “#lcfc magician @Mahrez22 commits future with new deal to 2020!.”
Mahrez alifanikiwa kuibuka kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita huku akifanikiwa kuifungia timu yake ya Leicester City mabao 17 na kutoa pasi za mwisho zilizozaa mabao 11.
0 comments:
Post a Comment