Kanye West kufungua maduka 21 ya nguo, moja litapatikana Afrika



Rapa wa Marekani, Kanye West anatarajia kufungua maduka yake ya nguo 21 yaliyopo kwenye nchi tofauti tofauti duniani wikiendi hii. Maduka hayo yatakuwa kwa muda tu (pop up shops).






Moja kati ya maduka hayo litakuwa linapatikana nchini Afrika Kusini kwenye mji wa Cape Town. Kanye West ameamua kufungua maduka hayo baada ya maduka matatu aliyoyafungua New York, Los Angeles na Paris kuwa na mauzo mazuri.

kupitia mtandao wake wa Twitter, Yeezy ameandika, “21 PABLO STORES WORLDWIDE THIS WEEKEND LOCATIONS HERE.”


Kwenye maduka hayo zitakuwa zinapatikana nguo zake pamoja na vitu vingine vya brand yake. Sehemu nyingine ambapo yatapatikana maduka hayo ni pamoja na Uingereza, Berlin, Amsterdam, Atlanta, Boston, Chicago, Dallas, Detroit, Houston, Las Vegas, Singapore na nchi nyingine nyingi.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment