Zaidi ya Hekari 545 za misitu na Mashamba ya mazao zateketezwa kwa moto na watu wasiojulikana.


Zaidi ya Hekari 545 za misitu na Mashamba ya mazao zateketezwa kwa moto na watu wasiojulikana.




Zaidi ya hekari 545.5 za misitu ya hifadhi ya serikali,mashamba ya watu binafsi ya miti na mashamba ya mazao ya chakula katika maeneo mbalimbali ya wilaya tatu za Biharamulo, Bukoba na Muleba zilizoko mkoani Kagera zimeteketezwa kwa moto uliowashwa na watu wasiojulikana na kusababisha hasara kubwa.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu akizungumza amesema vitendo vya uchomaji wa moto vinavyofanywa na watu wasiojulikana katika mkoa huo vilivyoanza tangu mwezi Julai mwaka huu kuwa havitavumilika hivyo amewaagiza viongozi wote katika mkoa huo kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya uchomaji moto kwa kuwa kiongozi atakayeshindwa kuthibiti vitendo hivyo atawajibishwa.

Aidha,Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wananchi wampe ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake ya kulinda amani na usalama na kuhakikisha sheria zinazingatiwa kwa kuwa jukumu la kulinda na kuhifadhi rasilimali za taifa ni la kila mtu.

 Source ITV



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment