Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amejikuta katika vita vya maneno na wakala wa kiungo Yaya Toure baada ya kuto mjumuisha katika kikosi cha wachezaji 25 watakaoshiriki katika mechi za klabu bigwa barani Ulaya katika hatua ya makundi.
Guardiola alisema hatamteua mchezaji huyo hadi pale wakala wake Dimitry Seluk, atakapoomba msamaha kwa matamshi aliyotamka kwa vyombo vya habari.
Yaya Toure na wakala wake Dimitry Seluk
Wakala huyo amesema katu hatafanya hivyo na badala yake akasisitiza kwamba meneja huyo ndiye afanye kuomba radhi.
”Kwa nini ni muombe msamaha Guardiola? Sijui maneno ninayostahili kutamka kuomba radhi, kwa sababu sijafanya kitu chochote. Iwapo nitajihisi kuomba radhi, basi nitaomba radhi hiyo, lakini sihisi kufanya hivyo. Kile Guardiola anachokitaka hakitawezekana,” alisema Seluk kwenye Tv ya Sky Sport News.
Amesema meneja huyo amewakosea watu wengi akigusia mtangulizi wake Manuel Pellegrini na kisha kipa nambari moja wa Manchester City Joe Hart ambaye alilazimika kuondoka klabu hiyo majira ya joto baada ya kuachwa nje ya mipango ya Guardiola.
“Ni lazima awaombe radhi Yaya na Hart na Pellegrini. Guardiola anashinda mechi kadha na kuanza kufikiria kwamba yeye ni mfalme.”
Seluk amesema mteja wake, Toure ,33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Guardiola amesema iwapo Seluk atamuomba msamaha yeye, klabu hiyo na wachezaji wa timu hiyo hapo ndio Yaya atakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katika michezo yote.
“Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kweye kikosi,” Guardiola ameongezea.
Guardiol alikuwa kocha wmkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.

0 comments:
Post a Comment