Niyonzima aongoza mgomo wa mazoezi Yanga



Kocha wa klabu ya Yanga Mzambia, George Lwandamina, amekumbana na ugumu mkubwa kwenye kazi yake baada ya wachezaji kugomea mazoezi kutokana na kutolipwa mshahara wao wa mwezi Novemba.


Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima ameiambia mtandao wa Goal, wameona ni vyema wakagomea kufanya mazoezi ili kuushawishi uongozi waweze kuwalipa mishahara yao ili kuweza kujikimu kimaisha.

“Nikweli hii ilikuwa ni makubaliano ya wachezaji wote ndiyo maana jana jioni tulikwenda mazoezini lakini hatukufanya mazoezi na leo kama tulivyofanya leo asubuhi, amesema Niyonzima.

Kiongozi huyo wa wachezaji amesema maisha yamekuwa magumu na wao wanategemea mishahara yao ili kuweza kupata huduma mbalimbali hivyo kufanya hivyo wanaamini uongozi wa Yanga utawasikiliza na kulipatia ufumbuzi haraka.

Alisema uongozi unapaswa kuangalia kilichopo mbele yao ambapo timu yao inakabiliwa na ushindani mkali wa kupigania ubingwa kati yao na wapinzani wao Simba hivyo nivyema wakawaanda kisaikolojia wachezaji ili waweze kupambana katia mechi zao kuliko kufanya hivyo.

“Namna hiyo inaweza kuwakatisha tamaa baadhi ya wachezaji hasa wale wapya waliosajiliwa hivi karibuni lakini tunaimani na uongozi wetu watapambana ili kulimaliza hilo,” amesema Niyonzima.

Kwaupande wake Kamaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Baraka Desidediti amesema kwasasa wapo katika mchakato wa kulifanyia kazi hilo na muda siyo mrefu watamaliza tatizo hilo la kuchelewa kwa mishahara.

“Nikweli wachezaji tulikuwa hatujawalipa lakini tatizo hilo lilitokana na muingiliano wa baadhi ya mambo hasa kwenye dirisha dogo la usajili lakini tayari taratibu za kuwalipa mishahara yao zinaelekea kukamilika na kesho asubuhi wachezaji wanaweza kuwepo mazoezini,”amesema Baraka.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani Ijumaa ya wiki hii kupambana na African Lyon, katika mchezo wa pili wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

Source: Goal.com


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment