Picha/Video: Darassa, Hanscana wanusurika kwenye ajali mbaya ya gari




Rapper Darassa, muongozaji wa video za muziki nchini, Hanscana na watu wengine wawili, wamenusurika kwenye ajali mbaya ya gari wakati wakiwa njiani wakitokea Kahama mkoani Shinyanga kwenda Kakola mkoani humo kwaajili ya show.




Gari namba T503 DGQ mali ya Hanscana ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali

Hakuna aliyeumiwa kwenye ajali hiyo iliyotokea mchana wa Jumapili (December 18), ingawa gari hiyo inayomilikiwa na Hanscana imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa Darassa, walikuwa wakiendesha kwa mwendo wa kawaida tu wakati ajali inatokea.








Kwenye speed 60 free road lakini icho kilicho tokea miujiza lakini MUNGU ana miujiza yake pia Mimi na director wangu @hanscana_ producer @mrvs2016 @abbah_process Wote tuko Poa 🙏🏽 CAN I GET AMAN FOR THAT 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽 #muziki,” ameandika Darassa kwenye Instagram.

Wengine waliokuwemo kwenye gari hilo ni rapper Mr VS na producer Abbah.

Rod accident BUT WE GOOOOOOOD 🤐 “My self @darassacmg @abbah_process @mrvs2016 #MUZIKI God Made thank you,” ameandika Hanscana.



Abbah, Mr Vs, Darassa na Hanscana wote wamenusurika kwenye ajali hiyo

“MUNGU ni mkubwa sana ameamua kututoa salama Kabisa kwenye ajali hyo mmi na Team Yangu @darassacmg @hanscana_ @mrvs2016 na mmi mwenyewe MUNGU MKUBWA,” ameandika Abbah.

Mastaa mbalimbali wametumia mitandao ya kijamii kuwapa pole. Hawa ni baadhi yao:

Diamond:

Poleni sana wanangu… Mwenyez Mungu aendelee kuwalinda, kuwaongoza vyema na kuwapa afya zaidi, mzidi kupambana @hanscana_ @Darassacmg
Harmonize:

Pole sana my brother @darassacmg & @hanscana_ Mungu ana miujiza yake tumshukuru kwa kila jambo…..🙏🙏 kwakuwa tupo wazima basi harakati ziendele…….!!!!
Izzo Bizness:

Poleni sana ndugu zangu kwa hili hakika MUNGU ni mwema 🙏 @hanscana_ @darassacmg @abbah_process
Chini ni picha zaidi:








Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment