Siri ya mahusiano ya Drake na Jennifer Lopez yaanza kuvuja



Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa sasa Drake na Jennifer Lopez wakawa na mahusiano ya kimapenzi.



Jumatatu hii Drake alifanya sherehe fupi kwenye mgahawa wa Delilah uliopo West Hollywood na J Lo alikuwa ni mmoja kati ya wageni muhimu 20 walioalikwa kwenye sherehe hiyo.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao huo kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ila kinachosubiriwa ni muda muafaka wa kuweka kila kitu wazi.

Kuna uwezekano mkubwa wawili hao wakawa na mahusiano kwa kuwa kwa sasa kila mmoja hana mpenzi ambapo J Lo alimpiga chini ex wake Casper Smart miezi mitatu iliyopita, naye Drake alidaiwa kuachana na Rihanna zaidi ya mwezi mmoja uliopita.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment