Romelu Lukaku kuweka rekodi mpya Everton



Mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku anatarajia kupewa mkataba mpya na klabu hiyo ya Everton ambao atakuwa akilipwa pauni 100,000.



Kiwango hicho cha malipo, kitamfanya Lukaku ambaye ni raia wa Ubelgiji ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Everton kulipwa kiasi hicho kwa wiki.

Everton ambayo uwanja wake wa nyumbani ni Goodison Park ambao upo jijini Liverpool, haijawahi kutoa pauni 100,000 kwa mchezaji yoyote.

Lukaku ambaye alijiunga na Everton Juni, 2019 akitokea Chelsea na imeelezwa wakala wake Mino Raiola amekuwa katika mazungumzo mazito na uongozi wa Everton.

Majira ya joto, nusura Lukaku arejee tena Chelsea lakini suala hilo lilishindikana baada ya mwekezaji mpya wa Everton, Farhad Moshiri kusisitiza anataka bado aendelee kubaki.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment