Tiny aomba talaka kwa mumewe rapper T.I.


Mwaka 2016 unaondoka na ndoa nyingine iliyoonekana imara kwa macho ya wengi. Ndoa ya T.I. na mkewe Tiny imefikia ukingoni.



Baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka sita, Tiny, muimbaji wa zamani wa kundi la Xscape, ameomba talaka kutoka kwa mume wake mwezi huu. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, uhusiano wao uliingia dosari zaidi baada ya kusambaa mtandaoni picha ya Tiny akicheza muziki na Floyd Mayweather, adui mkubwa wa T.I, kwenye party ya Halloween ya Mariah Carey.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2010 na pamoja wana watoto watatu, King, Major, na wa kike Heiress Harris, aliyezaliwa March. Licha ya kuachana, E! News inadai kuwa wataendelea kuwa marafiki kwaajili ya watoto na familia yao.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment