Mkhitaryan azunguzia goli lake la ‘Scorpion’



Mchezaji wa klabu ya Manchester United ambaye ni raia wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, baada ya kufunga bao ambalo limekuwa gumzo.



Mkhitaryan alifunga bao hilo wakati Man United ikiifunga Sunderland kwa mabao 3-1.



Bao hilo ambalo limepewa jina la “Half Scorpion”, alilifunga kwa kupiga kutumia unyayo wake wakati ikionekana kama mpira umempita.

Watau wengi wamekuwa wakijadili goli hilo hasa wakijadili mambo mawili. Wako wanaosema ni offside na wengine wamekuwa wakizungumzia ubora wake na kumpongeza Mkhitaryan.



Henrikh amezungumza na mwandishi wa habari kuhusu goli lake hilo. Amesema

“Lilikua ni goli bora niliwai kufunga, nilijiskia vizuri baada ya kulifunga na baada ya hapo nikamuangalia refa msaidizi na haikua offside nikaanza kushangilia.”

“Nilikua nategemea mpira mbele yangu, lakini nilikua tayari nipo mbele ya mpira, sasa sikua na jinsi zaidi ya kuupiga kwa nyuma na nikafanikiwa kuupiga.”

“Nashkuru mungu kwamba niko salama nimerudi nipo vizuri, sina maumivu yoyote baada ya kuumia siku zilizopita. Nafurahi kuwa sehemu ya timu na kusaidia kwa kadri niwezavyo.”

Alimzungmzia Zlatan na kusema “Haijalishi ana umri gani, kinachofanyika sasa hivi kila mtu anakiona. Yeye ni mchezaji mkubwa na kila mtu anafurahia anachokifanya hatuhitaji kuzungumzia sana kuhusu Zlatan.”



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment