Habari njema kwa mashabiki wa Liverpool kuhusu Coutinho



Mchezaji wa klabu ya soka ya Liverpool, Philippe Coutinho hatimaye amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya ku saini mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamalizika mwaka 2022.



Mkataba huo unaonyesha kuwa mchezaji huyo atakuwa akipokea mshahara wa paundi 200,000 na kumfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya timu hiyo kwa sasa. Coutinho alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na vilabu vikubwa vya Ulaya ikiwemo Barcelona.



Mpaka sasa mchezaji huyo aliyesajiliwa Januari 2013 akitokea Inter Milan ya Italia amesha cheza jumla ya mechi 163 akiwa na Liverpool na kuifungia magoli 34.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment