Madee amemchana Nay wa Mitego kwamba hana uwezo wowote kwenye muziki





Madee


Msanii wa Bongo fleva kutoka kitaa cha Manzese ambaye ndiye anayetambulika kama Rais wa Manzese, Madee, amemchana mwenzake kutoka kitaa hicho, Nay wa Mitego kwamba hana uwezo wowote kwenye muziki.

Madee akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV ambacho huruka LIVE kila Ijumaa Saa 3:00 usiku, aliamua kujibu mashambulizi ya Nay kwa kumrushia makombora mazito kutokana na Nay kudai kuwa ngoma mpya ya Madee ni ya kichovu na kwamba imeonesha ni jinsi gani Madee hana uwezo wa kuandika.

Katika majibu yake, Madee ambaye alikuwa akitambulisha kwa mara ya kwanza video ya ngoma hiyo ya ‘Hela’ alisema hata yeye haijui wala hajaisikia ngoma mpya ya Nay inayokwenda kwa jina la ‘Sijiwezi’ na kusema “Hiyo ngoma yake mpya siijui, wala sijaisikia maana nilikuwa nilikuwa nje muda mrefu….”

Baada ya kauli hiyo, ilibidi agongewe ngoma hiyo muda huohuo na DJ Summer ambaye ndiye aliyekuwa kwenye ‘mashine’, jambo la kushangaza, baada ya Madee kuisikia ngoma hiyo, aliiponda na kusema ni mbaya sana na haina hadhi ya kuimbwa na msanii mkubwa maana ni kama uchafu.
“Huo wimbo nausikia kama wa zamani sana, kama wa underground flani hivi, Sitaki kusikilizishwa tena huo uchafu” Alisema Madee.

Madee alisisitiza kuwa ngoma pekee ambayo ni nzuri kutoka kwa Nay, ni ile aliyoimba na Diamond (Muziki Gani) kwa kuwa aliimba na Diamond na pia aliiga mawazo yake Madee.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment