Sunderland yamsajili Lescott


Klabu ya Sunderland imemsajili beki wa zamani wa Aston Villa Joleon Lescott kwa mkataba wa muda mfupi.



Lescott ambaye ana umri wa miaka 34 , ambaye alikuwa akicheza chini ya meneja wa The Black Cats David Moyes huko Everton kati ya mwaka 2006 na 2009, amejiunga na klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu.

Lescott ambaye alimaliza mkataba wake na Aston Villa majira ya mwisho baada ya kushiriki msimu mmoja kwa klabu hiyo.
Baadaye alijiunga na AEK Athens, na kushiriki mechi nne na klabu hiyo ya Ugiriki kabla ya kupata jeraha na mkataba wake kufutiliwa mbali mwezi Novemba.

Sunderland ambayo iko katika nafasi ya mwisho katika jedwali la ligi ya Premia , wakiwa na alama 15, alama tatu juu timu zilizo hatarini kushushwa daraja.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment