Oscar 2017: Waigizaji Weusi wakumbukwa


Baada ya nomination za mwaka jana za tuzo za filamu za Oscar kusababisha mjadala mkubwa na kuwepo kwa hashtag #OscarsSoWhite, macho yote yalikuwa kwenye majina yaliyotajwa Jumanne hii.




Denzel Washington na Viola Davis

Habari njema ni kuwa tuzo za mwaka huu zimezingatia makundi madogo nchini humo. Katika miaka miwili iliyopita, hakuna mtu mweusi au jamii tofauti na wazungu aliyekuwa ametajwa kwenye vipengele vya uigizaji.

Lakini mwaka huu katika kila kipengele cha uigizaji, mtu wa jamii ndogo amejumuishwa. Waigizaji weusi saba wametajwa mwaka huu.

Kwenye kipengele cha muigizaji bora, yupo Denzel Washington kupitia filamu yake, Fences, na hivyo kuwa na rekodi ya muigizaji mweusi aliyewahi kutajwa mara nyingi kuwania kipengele hicho.

Muigizaji mwenzake, Viola Davis naye ametajwa kuwania tuzo ya muigizaji msaidizi wa kike. Wengine ni pamoja Octavia Spencer na Naomie Harris.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment