Nikki Mbishi aitwa BASATA kujieleza kuhusu wimbo wake ‘I am sorry JK’


Msanii wa muziki wa hip hop Nikki Mbishi amedai amepokea taarifa ya kuitwa na Baraza la Sanaa Taifa ‘BASATA’ kwajili ya mazungumzo kuhusu wimbo wake uitwao ‘I am sorry JK’.




Rapper huyo amedai aliitwa toka February 9 lakini alichelewa kupokea taarifa kwa kuwa alisafiri kwajili ya mazishi ya mama yake mkubwa.

Nikki kipitia Instagram yake ametoa taarifa hii

Salaam Tanzania,Afrika na Dunia!
Leo tarehe 13/02/2017 nimehitajika kuripoti ofisi za BASATA ambapo wanadai walinitumia ujumbe zaidi ya siku 3 nyuma ila sikuwa hewani labda kwa sababu ya msiba ulionipata, kufuatia ujumbe niliyotumiwa juzi tarehe 09/02/2017 kwa njia ya msg za kawaida za simu ya kiganjani ambapo
ujumbe umesema hivi “Habari za jioni?Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa ” I AM SORRY JK”
Nimeomba niripoti leo kufuatia kuchelewa kufika kwa ujumbe huo.
Unadhani nini kitatokea?Mi sifahamu ninachofahamu ni Itika wito kataa neno.
Asanteni na Mungu awabariki nyote.
#TagWaTanzania
#TagWaTanzania #TAGVIUMBEHAIWOTE #TAGVIUMBEHAIWOTE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment