Chris Brown akwama nchini Ufilipino, uhamiaji wamtilia ngumu


Chris Brown ameendelea kusugua gaga nchini Ufilipino kwa siku kadhaa sasa baada ya uhamiaji kumtilia ngumu kuondoka nchini humo.



Muimbaji huyo wa Loyal alijaribu kuondoka siku chache zilizopita lakini kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ndege aliyokuwa amepanda ilisimamishwa kabla haijapaa. Ni kutokana na masuala ya kisheria ambapo alikuwa atumbuize kwenye show ya mkesha wa mwaka mpya mjini Manila. Kwa mujibu wa waandaji wa show, alilipwa dola milioni moja lakini hakwenda kutumbuiza.

Waandaaji hao wanataka walipwe mpunga wao na wameiomba serikali isimruhusu aondoke mpaka awalipe.



Brown amepost picha kwenye Instagram akiwa amepiga magoti kusali na kuandika,” Please, please let us leave!”

Amemuomba pia Rais Barack Obama amsaidie.






Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment