
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, 2013 na msanii wa muziki Feza Kessy amezungumzia matarajio yake baada ya kupata uongozi mpya unaosimamia kazi zake.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Feza alisema kuwa chini ya usimamizi ni wazi atafika mbali zaidi.
“Nimesign contract yes. Sio kama watu wanavyodhani though. Sijasign contract with a new label, NO,” amesema.
“It’s just a new management team, meaning they handle my affairs concerning my music for example bookings, kutafuta shows/events, endorsement deals na vitu kama hivyo. Matarajio yangu ni wao kama kampuni kunisaidia kufika another level, after all siwezi kufanya kila kitu peke yangu,” ameongeza.
Pia Feza amezungumzia safari yake ya Kenya pamoja na ujio wa kolabo yake na Chege aliyeenda naye nchini Kenya hivi karibuni.
“True nilikwenda na Chege, he had some projects there, na as you know nimefanya kazi na Chege which I will release soon. I also got to work with some artists in Kenya. Kwa sasa ninarekodi sana more than anything then vingine vitafuata after that. Mashabiki wangu watarajie great music coming from me. I will release a series of few song in a couple of weeks, so wakae tayari tu. I hope they can be patient and support the good music that’s coming soon,” amesisitiza.
0 comments:
Post a Comment