Nisher na Vanessa Mdee wasifia uthubutu anaofanya Hemedy PHD

Hemedy PHD si msanii unayemsikia sana kwenye redio japo ni miongoni mwa waimbaji wazuri wa R&B, lakini kitu kimoja ambacho hupaswi kumnyima ni namna anavyojipanga kwenye video zake.






Hemedy akiwa kwenye location ya video yake Umebaki Story iliyofanyika kwenye mikoa minne nchini na kugharimu takriban shilingi milioni 15
Vanessa Mdee na Nisher wamemmwagia sifa staa huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu.

“Napenda unavyothubutu @hemedyphd you’re constantly reinventing yourself and taking risks. Ndivyo inavyotakiwa Mimi ni shabiki wako. I see you bro,” ameandika Vanessa kwenye Instagram.


Video ya wimbo huo uliotayarishwa Sei Records imefanywa na Kwetu Studios itatoka July 30. “I am still proud kushoot bongo sababu locations kali tunazo,” Hemedy ameiambia Bongo5.

“Nahamasisha wasanii wenzangu kutumia more nyumbani na kupatangaza pia,” ameongeza. Amesema video hiyo imefanyika kwenye mikoa ya Arusha, Morogoro, Dar es Salaam na Manyara na kwamba imemgharimu takriban shilingi milioni 15.


“Thank God niliweka malengo ya kufanya kitu kizuri home, nafikiri ni video yenye kiwango kizuri na inaitangaza Tanzania pia sababu nimetumia sehemu kubwa kuonyesha uzuri wa nchi.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment