Klabu ya Dar es Salaam Young African imezidi kujiweka kwenye nafasi nzuri katika michuano ya Kombe la KAGAME ambalo linaendelea Dar Es Salaam… Yanga ambayo ilianza mashindano hayo vibaya imeshacheza mechi tatu hadi sasa na kupoteza moja dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ambayo iliwafunga goli 2-1.
July 24 2015 Yanga imetinga Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na KMKM
ya Zanzibar ambapo Yanga imejiweka vizuri baada ya kuifunga KMKM ya
Zanzibar kwa jumla ya goli 2-0, huu ni mchezo ambao umemfanya Malimi Busungu kuingia
tena katika headlines baada ya kupachika goli la kwanza dakika ya 56
huku bao la pili KMKM wakijifunga wenyewe dakika ya 72.
Yanga ipo nafasi ya tatu katika kundi A kwa point 6 nyuma ya Al Khartoum ya Sudan na Gor Mahia ya Kenya, huku KMKM ya Zanzibar ikiwa nafasi ya nne na Telecom ya Djibout kushika mkia kwenye Kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment