Lakini kama unamfata Belle 9 katika mitandao ya kijamii, sina shaka utakuwa umekutana na post zake za jana na leo aki-tease kuwa kuna kazi mpya inakuja .
Moja inasomeka “Kitu kizuri kinakuja, kaeni mkao wa kula”, na nyingine “Get ready my people #loading….”. Mara nyingi Kwa msanii akiandika hivi humaanisha kuna kitu kinakuja muda mfupi ujao, kama siku mbili tatu au wiki.
Belle 9 mwenye makazi yake mjini Morogoro, ameiambia Bongo5 kuwa post hizo hazimaanishi kuwa ana kazi mpya anayotarajia kuitoa kwasasa, bali anamaanisha uwepo wake jijini dar na kuwaandaa watu na kazi zitakazokuja kutoka baada ya uchaguzi.
“Nilifanya Interview East Africa nikawaambia kwamba siwezi kufanya kitu chochote kwa saizi kwasababu naona mambo ya siasa yamechukua sana nafasi kubwa kwa watu wengi hususan wateja wetu…Kitu ambacho naki-tease ni kwamba mimi niko Dar kwa sasa, na kama unavyojua mimi ni msanii wa mkoani kwahiyo kama niko Dar kuna sehemu ambazo nikenda, huwa napenda watu wangu wajue kwamba niko Dar na niko sehemu fulani, kwahiyo kitu kizuri kinakuja hata kama sio kwa kipindi hiki labda yakishap ita mambo haya ya siasa. Ni kama attention hata kama sio ya sasa hivi napenda tu wadau pamoja na watu wote wanaohusika na maswala ya social networks wajue Belle 9 yuko around na yuko sehemu Fulani sasa hivi”. Alimaliza Belle 9.
0 comments:
Post a Comment